Monday, 17 July 2017

Aguero nae awaniwa na Conte

Baada ya kufanya usajili wa wachezaji watatu ambao ni Antonio Rudiger, Willy Caballero na Tiemoue Bakayoko lakini Conte bado hajaridhika, na sasa bado anaendelea kutafuta wa kuziba pengo la Diego Costa anayetazamiwa kuondoka muda mfupi ujao.
Sasa Conte amewafata wababe wa Manchester klabu ya Man city na kupeleka maombi ya kumsajili Kun Aguero ambapo inasemekana kocha wa klabu hiyo amekubali na sasa kinachobaki ni kufanyika makubaliano kati ya timu hizo mbili.
Mwandishi mmoja alituma katika mtandao wa Twitter akielezea ofa hiyo kwamba Chelsea imepeleka ofa kwa mchezaji huyo na inaelezwa kocha Pep amekubali kumuachia mshambuliaji huyo.
Muargentina huyo mwenye miaka 29 alisajiliwa na klabu hiyo mwaka 2011 na mpaka sasa ameichezea klabu hiyo jumla ya michezo 181 na ameifungia magoli 122.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.