Mshambuliaji na winga wa Leicester city, Riyad Mahrez bado hajajua hatma yake inakuwaje.
Mahrez ambaye alikuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu Uingereza msimu wa 2015-2016 amekuwa bado anapatwa na kigugumizi juu ya hatima yake klabuni hapo ikiwa tayari ashaomba kuondoka.
Tottenham na wao wameingia kwenye vita na majirani zao, Arsenal juu ya kumsajili mchezaji huyo ambaye Leicester inataka Paundi milioni 50 ili kumwachia nyota huyo.
No comments:
Post a Comment