Mshambuliaji na winga wa Leicester city, Riyad Mahrez bado anaiumiza kichwa Arsenal ambayo imekuwa ikimuwania kwa muda mrefu.
Arsenal ilitia dau ambalo lilitupiliwa mbali na mabingwa wa Epl msimu wa 2015-2016 ambapo Arsenal iliweka mezani kiasi cha Paundi milioni 40.
Lakini pia kuna dau jengine lililotolewa na klabu ya AS Roma iliyoweka mezani Paundi milioni 21 lakini Leicester city ikalikataa kabisa. Klabu hiyo inasema inahitaji kiasi cha Paundi milioni 50 ili kumuachia mwarabu huyo.
No comments:
Post a Comment