Huenda wananchi wa nchi moja wakabadilishana milango ndani ya Chelsea. Yani mmoja akatoka na mwengine akaingia.
Unajua ni nani? Mzee Llorente anaweza akaingia akampisha Diego Costa ambaye haonekani kuendelea kuwa na nafasi ndani ya klabu hiyo.
Unajua ni nani? Mzee Llorente anaweza akaingia akampisha Diego Costa ambaye haonekani kuendelea kuwa na nafasi ndani ya klabu hiyo.
Diego Costa alishaambiwa na Conte kwamba hayupo kwenye mipango yake na haitarajiwi kuonekana akiendelea kubaki, wakati Conte aliwai kupeleka maombi ya kumsajili kikongwe Llorente katika klabu ya Swansea ambayo ndio ana mkataba nayo.
Lakini kwa kuwa maombi aliyapeleka wakati ligi ikiwa inaendelea na Swansea haikuwa vizuri basi wakaamua kumkatalia Conte ofa yake juu ya kikongwe huyo ili timu iyo ipambane kutokushuka daraja.
Lakini kwa mshambuliaji tegemeo wa Chelsea, Diego Costa ambaye msimu uliopita alifanikiwa kutumbukiza mipira mara 20 katika Ligi kuu Uingereza wakati kikongwe wa Swansea akitumbukiza mara 14 lakini kwa wote ni kama hawatoendelea kubaki katika klabu zao, inategemewa hivo.
Costa anaitaka klabu yake ya zamani ya Atletico Madrid ambapo mpaka sasa ni kama analazimisha uhamisho wake wa kwenda klabuni hapo ukamilike ingawa klabu yake hiyo imefungiwa kusajili mpaka mwezi januari mwaka 2018.
Wakati hayo yakitokea kwa Costa, Antonio Conte anamtaka kikongwe huyo wa Swansea, Llorente ambaye waliwai kuwa pamoja katika klabu ya Juventus. Conte akiwa kama kocha. Lakini usajili huu unaonekana kuwepo baada ya Lukaku ambaye Conte alikuwa anamtaka kutangazwa kuungana na Man utd.
No comments:
Post a Comment