Bakayoko, 22 ambaye amesajiliwa rasmi na wababe wa London akitokea As Monaco ya Ufaransa kwa dau la Paundi milioni 40 amefichua kile alichoambiwa na kocha wake mpya, Antonio Conte baada ya kuonana mara ya kwanza mazoezini katika uwanja wa Cobham.
"nilipokutana nae tuliongea vingi haswa kuhusu mbinu za mpira na njia zake lakini pia alinambia nahitaji kufanya kazi kwa bidii na kudhihirisha ubora wangu" alisema Bakayoko akielezea kile alichoambiwa na muitaliano huyo.
"Chelsea ni klabu kubwa Uingereza, na itabaki kuwa hivyo na najivunia kuwa hapa lakini pia najivunia kuwa chini ya kocha bora (Conte)" aliongezea mchezaji huyo ambaye amesajiliwa kwa miaka mitano klabuni hapo.
No comments:
Post a Comment