Kiungo wa Man utd ambaye msimu uliopita alikuwa mchezaji bora wa ndani ya klabu hiyo, Ander Hererra amesema atakifanya kila atakachoweza kumbadilisha mawazo mhispania mwenzake De Gea.
David De Gea ameibuka na kulazimisha usajili wa yeye kujiunga na klabu mabingwa wa kihistoria wa Ligi ya Mabingwa Ulaya maarufu kama Uefa Champions, Real Madrid ufanyike haraka iwezekanavyo akioneshwa kutopendezwa tena kuendelea kubaki klabuni hapo.
Na ndio maana kiungo huyo, Hererra ameamua kusema atafanya chochote atakachoweza kumfanya De Gea abadili mawazo ya kuondoka klabuni hapo.
No comments:
Post a Comment