Monday, 17 July 2017

Costa ni kama tayari ashatua Atletico

Ndiyo! Jamaa ni kama tayari ashatua Atletico.

Hii ni mara baada ya kufanya video ya moja kwa moja katika mtandao wa Instagram akiwa na kikundi cha mziki mahali flanu huku yeye mwenyewe Diego Costa akiwa amevaa jezi ya Atletico Madrid ambapo kumekuwa na mawasiliano baina ya Diego Costa na upande wa klabu yake hiyo ya zamani.

Diego Costa ambaye ameisaidia Chelsea kutwaa mataji ya Ligi kuu Uingereza maarufu kama Epl mara mbili katika misimu mitatu na kombe la ligi maarufu kama Capital One amekuwa hana mahusiano mazuri na kocha wa sasa wa Chelsea, Antonio Conte na miezi kadhaa iliripotiwa kwamba Conte kamwambia mchezaji huyo kwamba hayupo kwenye mipango yake.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.