Hivi ulishawai kujiuliza Chelsea imetokea wapi? Hivi unajua nani alipambana kuihangaikia Chelsea mpaka kufikia hapa? Hivi unajua kuna mtu alijitoa kuifanya Chelsea iwe hapa ilipo ingawa alisemwa sana? Unamjua ni nani?
Kuna jamaa ambaye sasa ni marehemu ambapo alikuja duniani mwaka 1873 na akaaga dunia mwaka 1912, anaitwa Henry Mears ila kwa umaarufu ukitaja Gus mears tu unaeleweka maana alikuwa mtu mashuhuri ambapo nia yake ya kuanzisha klabu bora na kubwa duniani, Chelsea ulikuja baada ya viongozi wa klabu ya Fulham waligoma kuhamia kwenye uwanja wa Stamford Bridge ambao Mears alikuwa kama ana umiliki uwanja huo.
Baada ya viongozi wa Fulham kumgomea Mears akaamua auuze uwanja huo katika kiwanda cha makaa ya mawe kabla hajauuza uwanja huo ndio akapata wazo la kuianzisha klabu bora duniani, klabu ya Chelsea.
Mpaka anaiaga dunia muheshimiwa huyo hakufanikiwa kushuhudia klabu hiyo ikitwaa taji lolote. Ambapo wakatia anafariki klabu hiyo na maendeleo yake yote yalikuwa chini ya binamu wake.
No comments:
Post a Comment