Saturday, 22 July 2017

Conte bado amtaka nyota mwengine

Kocha wa , Antonio Conte bado hajalizika na wachezaji wanne aliowasajili na sasa anatazamia kufanya usajili mwengine wa nyota matata.

Nyota huyo anayetazamia kumsajili ni yule nyota wa ambaye kwa sasa yupo na timu katika kujiandaa na msimu mpya, Alex Oxlade Chamberlain. Conte anamtaka kumchukua mchezaji huyo akitazamia kujiimarisha na michuano mingi katika msimu mpya ambayo Chelsea itashiriki lakini huku ikiwa bingwa mtetezi wa Ligi Kuu Uingereza.

Chamberlain ambaye alisajiliwa na klabu hiyo akitokea Southampton amekuwa na msimu mgumj katika kikosi cha Wenger na sasa anatazamia kuachana na klabu hiyo. Chamberlain, 23 anatarajia kufanya mipango rasmi ya kuachana na klabu hiyo mara baada ya kurudi katika michezo ya kirafiki ya kujiandaa na msimu mpya inayoendelea barani Asia, China.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.