Ndiyo! Kocha wa Chelsea, Antonio Conte bado anahitaji saini za nyota wengine licha mpaka sasa kutumia kiasi cha Paundi milioni 130 kuwanunua Antonio Rudiger, Tiemoue Bakayoko na Alvaro Morata lakini bado anataka wengine.
Kocha huyo amesema kati ya saini anazozitaka klabuni hapo ni ya mchezaji mwengine wa kihispania anayeichezea klabu ya Swansea, Fernando Llorente.
Conte alishawai kuitaka saini ya mchezaji huyo mwenye uraia wa Hispania kama nyota mpya wa klabu hiyo, Alvaro Morata lakini klabu ya Swansea iligoma kumuuza kwa vile ilihitaji kupambana kutokushuka daraja.
No comments:
Post a Comment