Mchana wa leo katika mishale ya saa tisa mchana kutakuwa na mchezo wa kirafiki kati ya Chelsea na vijana wenzao wa London, Arsenal katika uwanja wa Beijing National Stadium wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 91,000.
Chelsea itacheza michezo itatu katika kujiandaa na msimu mpya ambapo itaanza na Arsenal siku ya leo alafu baada ya hapo itamenyana na Bayern Munich siku ya tarehe 25 kabla ya kumaliza na Inter Milan tarehe 28 mwezi Julai.
Hapa nimekuwekea picha za wachezaji wa Chelsea wakiwa kwenye mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya baada ya kutua katika bara hilo la Asia nchini China.
|
No comments:
Post a Comment