Monday, 24 July 2017

Conte amtaka wajina wake

Kocha wa Chelsea, Antonio Conte amegeukia tena kwa wajina wake mwengine baada ya wiki kadhaa kumsajili wajina wake Antonio Rudiger.

Chelsea inahusishwa na mpango wa kumnasa mlinzi wa Inter Milan, Antonio Candreva mwenye umri wa miaka 30.

Conte anatafuta mlinzi wa kulia ambaye ataweza kucheza endapo Victor Moses akipata majeraha au akipumzishwa na kocha huyo alikuwa akimfukuzia Danilo aliyejiunga na Manchester city.

Candreva ambaye amefanikiwa kuifungia Inter mabao 6 na kutengeneza mengine 10 kwa msimu uliopita amehusishwa na kutua darajani na usajili huo unaonekana kukalibia kukamilika kwa maneno aliyoyatoa wakala wa klabu hiyo.

"Candreva ana furaha Inter. Na ana furaha na ujio wa kocha mpya (Spalleti) lakini kuhusishwa na Chelsea ni jambo jema" alisema wakala wa mchezaji huyo ambaye pia alishawai kuichezea klabu ya Lazio.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.