Nyota wa Chelsea, Cesc Fabregas amempa tahadhari nyota mpya wa kikosi hicho Alvaro Morata ambaye amenunuliwa kwa dau la paundi milioni 70.
"Kuamia katika klabu kubwa kama Chelsea na ukawa mshambuliaji ambao utacheza michezo mingi basi kila mtu atahitaji magoli mengi kutokea kwako. Kila mtu anakutazama wewe ufunge maana wewe ni mshambuliaji. Kwa hiyo watahitaji (Morata na Batshuayi) kujipanga ili kupigana kufanya kile wanachohitajika kukifanya" alisema Fabregas ambaye alishawai kucheza na nyota huyo wakiwa timu ya taifa ya Hispania.
"Chelsea itakuwa na michuano mingi ya kushiriki msimu ujao, na kama mshambuliaji wa kati timu nzima inakuangalia wewe kama utafunga. Hilo ndilo jukumu lako" aliongezea kiungo huyo mtaalamu wa kupiga pasi.
Alvaro Morata anategemewa kuingia moja kwa moja katika kikosi cha kwanza cha Chelsea mara baada ya mshambuliaji Diego Costa aliyekuwa klabuni hapo kwa misimu mitatu kuambiwa hayupo kwenye mipango ya kocha Antonio Conte.
Morata amejiunga na wachezaji wenzake wakiwa barani Asia kujiandaa na msimu mpya ambapo tarehe 25-Julai itamenyana na Bayern Munich katika mchezo wa kirafiki kabla ya kumaliza na Inter Milan siku ya tarehe 28-Julai.
No comments:
Post a Comment