Monday, 24 July 2017

Owen aipa ubingwa Chelsea

Gwiji wa soka wa zamani aliyewai kukipiga ndani ya Manchester united na Liverpool, Michael Owen ameitabiria Chelsea kuwa na moto uleule uliokuwa nao msimu uliopita.

Akihojiwa na kituo kimoja nchini Uingereza, Owen alisema "ingawa dirisha kubwa bado halijafungwa lakini naona nafasi ya Chelsea kuwa na moto ule bado ni kubwa"

Alisema nyota huyo wa zamani aliyetamba na klabu kubwa Ulaya kama Liverpool, Real Madrid na Manchester utd alipomalizia soka lake hapo.

Chelsea ipo barani Asia kujiandaa na msimu mpya ambapo mpaka sasa klabu hiyo imeshacheza michezo miwili ya kirafiki, ilianza na Fulham na kuibamiza 8-2 kabla ya kumaliza na Arsenal kwa kuifumua mabao 3-0.

Klabu hiyo imebakiza michezo mingine miwili kumaliza michezo hiyo ya kirafiki ambapo kesho itamenyana na Bayern Munich na tarehe 28 itamenyana na Inter Milan.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.