Saturday, 22 July 2017

Boga nyota wa Chelsea aliyewaduwaza wengi dhidi ya Arsenal

Jioni ya leo katika mchezo wa kirafiki uliowakutanisha Chelsea dhidi ya Arsenal nchini China, mchezo ambao umeishuhudia Chelsea ikitoka kimasomaso kwa jumla ya magoli 3-0.

Shukrani kwa magoli ya Michy Batshuayi aliyechaguliwa kuwa nyota wa mchezo huo ambapo amefunga magoli 2 na kutengeneza jengine lililofungwa na Willian.
Lakini katika mchezo huo gumzo kubwa lilikuwa kwa kijana wa Chelsea aliyeingia kuchukua nafasi ya Pedro aliyeumia katika dakika ya 29, Jeremie Boga.

Wengi wameshangazwa na uwezo wake wa kuuchezea mpira na kuwasumbua nyota wa Arsenal ambapo alimfanya vibaya mlinzi mpya wa Washika bunduki, Kolasinac na kiungo wa klabu hiyo Coquelin kwa chenga zake na uwezo wake mkubwa.

Baada ya mchezo huo kumaliza kumekuwa na gumzo kubwa haswa mitandaoni ambapo wengi wameshangaa mambo na uwezo wake mkubwa uwanjani.

Jeremie Boga ni nani?
Jeremie Boga ni raia wa Ufaransa aliyezaliwa katika jiji la Marseille nchini Ufaransa ambapo wazazi wake wote wawili wana asili ya Ivory Coast.
Alizaliwa tarehe 3 ya mwezi Januari mwaka 1997. Na anacheza nafasi ya kiungo lakini akimudu pia kucheza kama winga.

Ana historia gani katika soka?
Jeremie Boga alianza kucheza soka katika klabu ya ASPTT Marseille ya nchini Ufaransa na alijiunga na akademi ya Chelsea mwaka 2008 mara baada ya kusafiri na familia yake mpaka Uingereza katika jiji la London ambapo baba yake alikuwa akifanya kazi jijini hapo.
Alipandishwa mpaka timu ya wakubwa ya Chelsea na katika mchezo dhidi ya Sunderland katika msimu wa 2014-2015 alikuwa katika benchi kama mchezaji wa akiba mchezo ambao Chelsea ilishinda 3-1.
2015 akatolewa kwa mkopo kwenda Stade Rennais ya nchini kwao Ufaransa ambapo huko alicheza jumla ya michezo 28 na kufunga magoli 3 akicheza kama kiungo. Huko alicheza mpaka msimu wa 2015-2016 kabla ya kutolewa tena kwa mkopo na kwenda Granada ya Ufaransa ambapo napo uko alicheza michezo 26 na kufunga magoli 2.

Lakini pia kwa jambo ambalo hujalijua kwa Jeremie Boga kwamba jamaa kaichezea timu ya taifa ya Ufaransa U-16 na ya U-19 kabla ya kuamua kuichezea timu ya taifa ya asili ya wazazi wake yaani Ivory Coast.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.