Sunday, 23 July 2017

Chelsea yawaomba radhi wachina

Chelsea imeomba radhi wananchi na wapenda soka nchini China kwa kilichofanywa na nyota wa klabu hiyo, Kennedy ambapo wakati klabu hiyo ikiwa nchini humo kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya.

Kennedy alituma picha za mnato na huku zikifuatiwa na lugha ambayo iliwakera wachina wengi. Hali ilyowafanya uongozi wa Chelsea kutumia mtandao maarufu nchini humo kuwaomba radhi kwa jambo alilolifanya kinda huyo.

"Tunaomba radhi kwa kilichotokea kwa kauli iliyotolewa na mchezaji wetu, Kennedy" ni ujumbe uliosomeka katika mtandao huo ambapo Chelsea iliwaomba radhi wananchi wa China.

Chelsea ipo nchini China kujiandaa na msimu mpya ambapo jana ilimenyana na Arsenal katika mchezo ulioisha kwa Chelsea kuchomoza na ushindi wa mabao 3-0, magoli yakifungwa na Michy Batchuayi aliyefunga mara mbili na jengine likifungwa na Willian Borges.

Klabu hiyo itacheza tena mchezo wake wa tatu wa kirafiki baada ya Fulham na Arsenal itacheza na Bayern Munich siku ya jumanne ya tarehe 25-Julai

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.