Chelsea imemtaja tena Christian Benteke ambaye ni mshambuliaji wa Crystal Palace katika mpango wake wa kumsajili mshambuliaji atakayeziba pengo la Diego Costa, atakayeachana na mabingwa hao muda wowote kuanzia sasa.
Benteke ameingia katika orodha pale ambapo Chelsea inasaka mshambuliaji baada ya kukosa saini ya Romelu Lukaku aliyetimkia Man utd.
Wachezaji wengine wanaotajwa kuwaniwa na klabu hiyo ni Pierre Aubameyang, Kun Aguero, Andrea Bellotti na Alvaro Morata anayekaribia kutua AC Milan.
No comments:
Post a Comment