Baada ya Chelsea kukamilisha sajili za wachezaji wanne, Caballero, Rudiger, Bakayoko na sasa ni Morata kumekuwa na mapokeo makubwa juu ya ujio wa mshambuliaji huyo anayetegemewa kuchukua nafasi ya Costa.
Mchezaji Bakayoko ametuma picha akiwa na mshambuliaji huyo aliyesajiliwa kwa dau la Paundi milioni 58 wakiwa wote London huku Bakayoko akiandika maneno ya kumkaribisha.
Bakayoko hajasafiri na timu ambayo sasa ipo barani Asia ambapo itacheza michezo ya kujiandaa na msimu mpya. Hajasafiri na timu kwa kuwa ana majeruhi.
Kwa maana hiyo wachezaji hao walikutana katika uwepo wa Chelsea ambapo Morata ashatua London ili kukamilisha vipengele vya mwisho.
No comments:
Post a Comment