Monday, 10 July 2017

Bakayoko muda wowote atasaini Chelsea

Kiungo mwenye miaka 22 wa As Monaco, Tiemoue Bakayoko anatarajiwa kusaini ndani ya Chelsea muda wowote akimaliza kufanya vipimo vya afya ndani ya klabu hiyo ya Uingereza.

Bakayoko ambaye msimu uliopita ameisaidia Monaco kutwaa kombe la Ligi kuu Ufaransa maarufu kama Ligue 1 ambayo ilipita miaka 17 toka klabu hiyo kutwaa taji hilo amekuwa akitakiwa na Chelsea kwa karibu ili kutengeneza ushirikiano mzuri na mfaransa mwenzake N'golo Kante ambaye anategemea kumpoteza 'partner' wake kwenye kiungo, Nemanja Matic waliotumia msimu uliopita wakicheza pamoja.

Matic anatakiwa kwa karibu na Man utd ya Mourinho ambapo kwa ujio wa Bakayoko inaaminika itakuwa mkono wa kwaheri kwa Matic.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.