Baada ya As Roma kumuuza Antonio Rudiger kuja Chelsea kwa dau la £34 milioni sasa inaonekana ni zamu ya Radja Nainggolan kuachana na klabu hiyo, wakati Chelsea ikiwa inamfukuzia pia mchezaji huyo mwenye uraia wa Ubelgiji.
Katika mtandao wa Instagram, mchezaji nyota wa timu hiyo, Strootman alitoa ujumbe wa kumuaga mchezaji mwenzake huyo baada ya kuungana na nyota mwenzake wa timu hiyo, Mohammed Salah aliyesajiliwa na Liverpool wiki kadhaa zilizopita sasa Rudiger amesajiliwa na Chelsea. Mchezaji huyo aliandika "Ni huzuni kumuaga Rudiger, nahisi atakuwa mchezaji wa mwisho kwetu kuondoka (AS Roma)" ndipo baada ya muda Nainggolan aliupenda ujumbe huo na akatoa maoni au 'comment' kwa kuandika "sina uhakika kama kweli" akimaanisha hana uhakika kama Rudiger ndie mchezaji wa mwisho.
Wachambuzi wa soka wameitafsiri kauli hiyo kwamba huenda Nainggolan nae akaondoka muda wowote kuanzia sasa, Antonio Conte anamuwania mchezaji huyo.
No comments:
Post a Comment