Ndiyo! Kiungo wa kifaransa anayekipiga AS Monaco, Tiemoue Bakayoko amebakiza saa chache kuungana na Chelsea.
Kiungo huyo ambaye alitakiwa na Conte kwa muda mrefu ni kama tayari ashatua Darajani. Hii ni baada ya Chelsea kukubali dau la Monaco ambalo limepanda toka paundi milioni 35 iliyotajwa mwanzo kwamba ni thamani ya Bakayoko mpaka dau lake la sasa ambalo limetajwa kuwa ni paundi milioni 40. Dau ambalo Chelsea imekubali kulitoa na sasa kilichobaki ni Bakayoko kufungasha virago vyake na kutua Chelsea ili afanyiwe vipimo na kusaini katika klabu hiyo itakayoanza ratiba yake ya mechi za kirafiki tarehe 22 ya mwezi huu wa saba dhidi ya Arsenal katika bara la Asia.
{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater}
The moment you come is the moment we let you go away
{facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
No comments:
Post a Comment