Tangu kuwasili kwa Antonio Conte pale darajani basi yule mkali wa pasi wa kihispania Cesc Fabregas amekuwa hana uhakika wa kupata namba kikosi cha kwanza. Je unajua kwanini mkali huyu wa pasi za mwisho amekuwa hana nafasi sana kwenye daftari la Conte? Je kwanini Fabregas alikuwa na uhakika wa namba kwa Mourinho ila sio kwa Conte?
Sasa haya ndio majibu!
Fabregas ambaye ni raia wa Hispania kama utamaduni wa soka lao la Kihispania ni watu wa kucheza pasi nyingi na kutumia viungo kama wakabaji wao na washambuliaji pia. Soka la Kihispania maarufu kama tik tak limekuwa linatumia sana viungo kucheza pasi nyingi kwa maana hiyo inakuwa ngumu kwa adui kuupata mpira na kufanya mashambulizi. Huyo ndio Fabregas na soka lake la pasi za ufundi na uvivu wao wa kukaba au kuzuia.
Kwanini Fab haingii kwenye mahesabu ya Conte.
Wakati Conte anafika ligi kuu ya Uingereza alikuwa bado hajaelewa ni aina gani ya mfumo atumie ili aweze kupata matokeo chanya. Ni kweli alianza vizuri lakini hata mwenyewe (Conte) aliwai kukiri hakuwai kufurahishwa na Chelsea ilivyokuwa inacheza japo alikuwa anapata matokeo.
Akaamua kuja na mfumo wake wa kiitalia wa 3-4-3 mfumo ambao ni wa kukaba sana.
Na kwa maana hiyo aliitaji mawinga ambao wana kasi na viungo wanaoweza kukaba ili kuwapunguzia majukumu hao walinzi watatu wa nyuma.
Matic ndie mchezaji aliyeongoza kwa kuzuia (tackling) msimu wa 2014-2015 kwa maana hiyo ingekuwa ngumu kwa Fabregas kuwa chaguo la Conte mbele ya Matic.
Kante ndie aliyeongoza kwa kuzuia na kukata umeme (tackling and interceptions) katika ligi kuu Uingereza msimu wa 2015-2016 hata kipofu asingeweza kumweka nje ili Fabregas aanze.
Unadhani Fabregas atakuwa vipi bora mbele ya viungo hao.
Sababu kubwa ya Fabregas kuwa bora kipindi cha Mourinho kwa sababu Mourinho mara nyingi alikuwa anatumia mfumo wa 4-2-3-1 mfumo ambao hauhitaji viungo wakabaji wengi maana una walinzi wanne nyuma kwa maana hiyo Matic alikuwa anaweza kusimama na Fabregas peke yake pale kati kati na timu ikawa kwenye uwiano mzuri.
Kwa maana hiyo sio kama Conte hampendi au kutomkubali Fabregas, la hasha! Lakini utawekuwa na ujasiri gani wa kubadilisha mfumo uliokupa ushindi katika mechi 13 mfululizo (3-4-3) na kukuweka juu katika msimamo kisha uuweke mfumo uliokufanya ukapoteza points 8 katika mechi tatu mfululizo (Swansea 2pts, Arsenal 3pts na Liverpool 3pts)
"cha muhimu ni timu kupata matokeo mazuri na sio kumfurahisha mchezaji fulani" alisema Conte.
No comments:
Post a Comment