Leo ni tarehe 22-February-2017 ni kumbukumbu ya kuzaliwa ya mmoja kati ya wachezaji bora waliowai kutokea Chelsea, Branislav Ivanovic ambaye alizaliwa tarehe kama ya leo mwaka 1984 kwa maana hiyo anatimiza miaka 33 siku ya leo.
Ivanovic ambaye ni raia wa Serbia nchi ambayo pia anaitumikia akiwa kama nahodha wa timu, maisha yake ya soka alianziwa katika timu ya mtaani kwao ya Remont Cesak na kwenda tena FK Srem.
Lakini Chelsea walimsajili akitokea timu ya Lokomotiv Moscow ambayo ni timu pinzani ya timu anayoichezea kwa sasa Zenit Saint Petersburg.
Alisajiliwa na Chelsea mwanzoni mwa mwaka 2008 na kufanikiwa kuichezea au kuitumkia mpaka kusajiliwa na Zenit mwezi wa February mwaka huu 2017.
Chelsea walimsajili kwa dau la £ 9milioni (paundi milioni 9) na kufanikiwa kuichezea jumla ya michezo 377 na kuwa moja kati ya wachezaji watano kutokea nje ya Uingereza kucheza michezo zaidi ya 300 na kufanikiwa kuifungia jumla ya magoli 34.
Mpaka anaondoka Chelsea amefanikiwa kutwaa jumla ya mataji 8; mawili ya ligi kuu, matatu ya FA Cup, 1 la League cup, moja la Uefa Champions league na moja la Uefa Ueropa cup.
Usilolijua kuhusu Ivanovic, baba yake mzee Rade naye pia alikuwa mchezaji na alikuwa akicheza nafasi anayocheza mtoto wake kwa sasa ya ulinzi. Lakini pia kama haujajua Ivanovic alianzia kucheza kama mshambuliaji kabla ya kuhamishwa na kuanza kuwa mlinzi.
No comments:
Post a Comment