Inaaminika sababu kubwa iliyomfanya mwamuzi aliyetwaa tunzo kama refa bora kwa mwaka jana, Mark Clattenburg mwenye miaka 41 kuachana na soka la Uingereza na kwenda kufanya kazi hiyo ya urefa katika nchi ya Saudi Arabia ni mchezaji wa zamani wa Chelsea ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya China, mnigeria John Obi Mikel.
Ilikuwa kutokuelewana kumetokea na ndipo Obi Mikel alimfata refa huyo na kuanza kulalamika jambo juu yake na ndipo Clattenburg inasemekana akatoa maneno ya kibaguzi kwa mchezaji huyo.
Juan Mata ambae nae alikuwa karibu wakati Mikel akilalamika jambo kwa refa alisema alisikia refa huyo akimwambia Mikel "shut up you son of monkey" akimaanisha "nyamaza we mtoto wa nyani"
Na ndipo shutuma hizo zilifikishwa katika chama cha soka cha FA na kukabidhiwa chama cha marefa cha Uingereza kinachosimamia marefa cha PGMOL lakini chama hicho hakikuonyesha support yeyote kwa refa huyo. Hiyo ndio sababu kubwa inayoaminika iliyomfanya Clattenburg kuachana na soka la Uingereza na kutimkia Saudi Arabia ambapo sababu hiyo imeelezwa na mmoja wa marefa waliokuwa karibu na refa huyo katika kipindi cha sakata hilo, mpaka wiki ijayo anategemewa kuachana na Uingereza.
No comments:
Post a Comment