Wednesday, 22 February 2017

Bonucci njia nyeupe kukutana na Conte

Huenda ukawa ni wakati mwengine wa marafiki kukutana tena. Ndio marafiki! Ni Bonucci na kocha wake wa zamani ambaye walikuwa wote Juventus na timu ya taifa ya Italia.

Bonucci ambaye ni beki kisiki wa Juventus ambaye ameichezea timu hiyo kwa mafanikio makubwa amekuwa hana mawasiliano mazuri na kocha wake wa Juventus wa sasa Allegri ambapo kutokuelewana huko kumemfanya mpaka kocha huyo kutomjumuisha katika kikosi kitakachomenyana na FC Porto usiku wa leo katika kombe la Uefa na hali hiyo inaonyesha huenda Bonucci akatafuta mahali pa kwenda kuendeleza soka lake.

Bonucci ambaye amewai kufanya kazi na kocha wa sasa wa Chelsea, Antonio Conte kwanza wakiwa Juventus kabla ya Conte kuchaguliwa kuwa kocha wa Italia na huko pia kukutana tena wamekuwa wakionekana kuwa na uhusiano mzuri hali ambayo inatafsiriwa huenda Conte akamchukua mlinzi huyo mwenye miaka 29 kwa sasa.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.