Hatimaye mpira umeisha, na vijana wa Abramovich, Chelsea wamepeleka ushindi kwa kocha wao Antonio Conte.
Willian ndio alikuwa wa kwanza kuifungia Chelsea goli la kwanza kabla ya Batshuayi kufunga tena jengine na kuifanya Chelsea imalize kipindi cha kwanza ikiwa mbele kwa magoli 2-0. Lakini katika kipindi hicho cha kwanza kilimshuhudia winga wa Chelsea, Pedro Rodriguez akichezewa rafu mbaya na kipa wa Arsenal na kumfanya mhispania huyo kushindwa kuendelea na nafasi yake kuchukuliwa na kinda, Bogga.
Kipindi cha pili kilianza kwa Chelsea kufanya mabadiliko ya kadhaa kabla ya kushuhudia tena mshambuliaji aliyesajiliwa akitokea Olympique Marseille, Michy Batshuayi akifunga tena goli jengine akipokea pasi murua kutoka kwa Marcos Alonso.
Mpaka mpira unaisha Chelsea ilifanya mabadiliko ya kikosi chake chote na ikishuhudia wale wachezaji wa akiba na wengine wakitokea kwenye akademi wakicheza katika mchezo huo.
No comments:
Post a Comment