Sunday, 23 July 2017

Hii ndo sababu iliyomfanya Conte aachane na Costa

Baada ya maneno mengi juu ya Costa na Chelsea na juu ya kulazimisha kwake kuondoka klabuni hapo. Lakini pia ulishajua kilichotokea mpaka Conte kuamua kumtumia ujumbe mfupi kwa simu mhispania huyo na kumwambia ayupo kwenye mipango yake?

Sasa hapa nakupa majibu yote kwanini Conte aliamua kumtumia ujumbe huo mtu aliyeisaidia Chelsea kutwaa Ligi Kuu Uingereza katika msimu wa kwanza wa kocha huyo ndani ya Chelsea.

Conte alipoojiwa kuhusu sakata hilo alisema "hii ishu ilianzia toka mwezi januari, na ilishaeleweka kwamba Costa hatoendelea kuwepo, lilieleweka kwa timu, wakala wake na hata yeye mwenyewe (Costa)"

Mwezi januari ambao Conte anauongelea kulitokea tukio mazoezini ambapo Diego Costa aligomea kufanya mazoezi akisingizia ana tatizo mgongoni, hii ikamfanya Costa kugombana yeye na mmoja wa makocha wa timu hiyo.

Kwa hiyo toka tukio hilo litokee basi Conte akaamua msimu utakapoisha basi Costa atakuwa wa kwanza kuachana na klabu hiyo, na ndicho alichokifanya kocha Antonio Conte, muda ulipowadia akamtumia ujumbe mshambuliaji huyo kumtaarifu sasa hana chake klabuni hapo.

Diego Costa ameachwa na Chelsea ambayo ipo barani Asia ikijiandaa na msimu mpya, na Costa ameshaonyeshwa mlango wa kutokea mara baada ya Conte kumpata Alvaro Morata atakayechukua nafasi yake.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.