Monday, 24 July 2017

Fabregas kuingia kwenye mipango ya Conte

Kocha wa Chelsea, Antonio Conte ameongelea uwepo na uwezekano wa nyota Cesc Fabregas katika kikosi chake msimu ujao.

Kocha huyo amesema "ni mchezaji mzuri na anafanya vizuri kwenye mechi na hata mazoezini. Amekuwa mfano kwa wachezaji wenzake."

Mhispania huyo alikuwa hana nafasi ya uhakika katika kikosi cha kocha huyo msimu uliopita lakini baada ya kiungo huyo kufanya vizuri katika michezo ya kujiandaa na msimu mpya, kocha huyo ameamua kumwingiza kwenye kikosi cha kwanza.

"ana uwezo mkubwa, na atakuwa mchezaji muhimu katika kikosi changu msimu ujao. Ana uwezo wa kucheza namba 10. Msimu uliopita mzunguko wa pili alicheza michezo mingi na alitusaidia kutwaa taji la ligi kuu na kuisaidia klabu kufika fainali ya kombe la FA" aliongezea kocha huyo.

Alisema kocha huyo raia wa Italia ambapo ameisaidia Chelsea kutwaa kombe la ligi kuu msimu uliopita.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.