Sunday, 23 July 2017

Dau la Chamberlain kuwekwa mapema

Chelsea ambayo mpaka sasa imeshafanya usajili wa wachezaji wanne bado haijalizika na sasa imepanga kwenda kwa majirani wao katika jiji la London, Arsenal na kuweka dau kwa nyota wa timu hiyo Alex-Oxlade Chamberlain.

Chamberlain ambaye kwa sasa yupo na klabu yake hiyo nchini China amegoma kusaini mkataba mpya na klabu hiyo ambapo alipewa ofa ya kuongezewa mshahara mpaka kufikia Paundi 100,000 kwa wiki. Mkataba wa sasa wa mchezaji huyo na klabu ayke hiyo unaisha kipindi cha kiangazi mwaka 2018.

Chelsea imepanga kutia dau kwa mchezaji huyo ndani ya masaa 48 yajayo ambapo thamani ya mchezaji huyo inatajwa kufikia Paundi milioni 25.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.