Mshambuliaji mahiri mwenye uraia wa Hispania, Diego Costa amesema hayupo tayari kucheza China.
Mchezaji huyo ambaye alisajiliwa na Chelsea akitokea Atletico Madrid alipata taarifa kutoka kwa kocha wake wa sasa Antonio Conte kwamba hamuhitaji tena katika klabu yake na atafute pakwenda.
Kutokana na kauli hiyo, Diego Costa ameamua kurudi katika klabu yake ya mwanzo ya Atletico Madrid na hayupo tayari kwenda kucheza nchini China ambapo amekuwa akitakiwa pia.
No comments:
Post a Comment