Kuelekea mchezo wa West Ham dhidi ya Chelsea hapo jumatatu, kocha wa West Ham, Slaven Billic ametoa neno kuhusu mchezo huo. Alisema;
"mi ni shabiki wa Conte. Namfuatilia sana na hata alivyokuwa Juventus nimekuwa na mtazama na niliona atakuja kuwa kocha bora baadae. Napenda jinsi anavyohamasisha timu na sioni kama kutakuwa na mchezo rahisi kwa kuwa eti tulipata ushindi dhidi yao kwa mara ya mwisho.Ni jambo kubwa sana kuweza kuongoza kwa tofauti ya point 10. Timu yake imeimarika na wachezaji wanajiamini mimi na wachezaji wangu inabidi tupambane zaidi kuweza kupata matokeo mazuri" alisema Slaven Billic
Mchezo wa mwisho kwa Chelsea na West Ham kukutana katika kombe la ligi la EFL na West Ham kuchomoza na ushindi wa magoli 2-1.
No comments:
Post a Comment