Friday, 3 March 2017

Chelsea yang'aa tunzo za London mwaka 2017

Jana usiku wa alhamisi katika jiji la London kulikuwa na tunzo zinazotolewa kuhusu mpira wa miguu katika jiji hilo. Kukiwa na vipengele kadhaa ambavyo Chelsea ilifanikiwa kuingiza watahiniwa wake. Katika kipengele cha kocha bora wa mwaka 2017 alishinda Antonio Conte wa Chelsea ambaye alichaguliwa kocha bora huku akiwipiku wenzake kama kocha wa Tottenham aitwaye Mauricio Pochettino, kocha wa Millwall aitwaye Neil Harris, kocha wa Fulham aitwaye Slavisa Jokanovic na Neal Ardley wa AFC Wimbledon. Ambapo Conte ameshinda tunzo hiyo katika msimu wake wa kwanza.

Ambapo katika kipengele cha mchezaji bora wa mwaka 2017 kwa wanaume alishinda kiungo wa Chelsea, N'Golo Kante ambaye ameiongoza Chelsea kufanikiwa kuongoza katika msimamo wa ligi kuu ya Uingereza kwa tofauti ya point 10. Kante aliwashinda Diego Costa ambaye anacheza nae timu moja ya Chelsea, Alexis Sanchez wa Arsenal na Delle Alli pamoja na Danny Rose wote wa Tottenham, huku katika tunzo ya mchezaji bora chipukizi akichukua Delle Alli.

Lakini ikumbukwe kuwa tunzo hizo ni kwa ajili ya timu zinazopatikana katika jiji la London nchini Uingereza ambapo kama haujajua London ndio jiji lenye timu nyingi za soka kuliko miji yote Uingereza.

Timu zinazopatikana katika jiji hilo ni kama Chelsea yenyewe inayopatikana London magharibi katika barabara ya Fulham, na timu nyengine ni kama Arsenal, Tottenham, West Ham, Crystal Palace, Fulham, Millwall na nyengine nyingi.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.