Wednesday 8 February 2017

Terry muda wako ushafika

Beki wa zamani ambaye pia anatajwa kuwa kati ya wachezaji bora kutokea ndani ya Chelsea, Marcel Desailly amemwambia nyota wa Chelsea, John Terry kwamba anapaswa kuondoka kwenye timu hiyo maana hana nafasi tena kuwepo katika timu hiyo.

Desailly ambaye alikuwa beki kisiki aliecheza pindi ambapo Terry alikuwa bado kijana alisema
"kipindi kile walinizidi kasi, walikuwa bora zaidi yangu. Nami nikaona muda wa mwafaka umefika ili mimi niondoke niwaache na wao wapambane, nami nadhani naye sasa inabidi aondoke ili awaachie vijana na wao wapambane"

Terry amekuwa hana uhakika wa kuwepo katika kikosi cha kwanza toka Conte alipofika katika kikosi hicho, huku kwa sasa akiwa na miaka 36.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.