Kinda wa Chelsea aliyejiunga na Bristol city timu inayoshiriki ligi ya Championship ya Uingereza ambaye amerudi Chelsea kwa ajili ya kufanyiwa matibabu baada ya kupata majeraha, Tammy Abraham amesema mwanzoni wakati alipojiunga na timu hiyo aliyokuwa kwa mkopo amesema alikuwa ana nia nzuri tu.
"mwanzoni wakati wa msimu mpya kuanza nilipanga kufunga magoli 30 lakini kwa majeruhi haya yatasababisha nikose michezo miwili lakini bado naamini naweza kutimiza ndoto yangu"
Tammy Abraham ambaye amekuwa akicheza kwa kiwango cha juu kama mshambuliaji toka akiwa Chelsea ya vijana ana nia ya kupambana ili kuingia katika kikosi cha Chelsea kilicho chini ya Conte.
No comments:
Post a Comment