Saturday, 25 February 2017

PL; Chelsea vs Swansea 25-February

Kuelekea mchezo wa jioni ya leo, je wajua kocha wa sasa wa Swansea, Paul Clement aliwai kuwa kocha wa Chelsea?

Ndiyo! Maisha yake ya ukocha aliyaanzia katika shule ya soka ya Chelsea kwa mwaka 1995-2000 kabla ya kuondoka kwenda kuifundisha timu ya taifa ya Ireland U21 na kurejea tena Chelsea mwaka 2007 ambapo alikaa mpaka 2011 na kuwa kocha msaidizi kwa Carlo Ancelloti kabla ya kuondoka naye na kwenda kuwa msaidizi tena kwa Ancelloti ndani ya Real Madrid.

Kwa maana hiyo leo ni kama anarudi nyumbani yeye na msaidizi wake, Claude Makelele ambaye naye alikuwa bora sana ndani ya Stamford Bridge.

Leo jioni saa 18:00
Chelsea vs Swansea
Uwanja wa Stamford Bridge

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.