Saturday, 25 February 2017

Lukaku bado ana hamu na Uefa

Mchezaji mwenye uraia wa ubelgiji anayejumuisha kikosi cha dhahabu cha wachezaji wa kibelgiji wanaocheza katika ligi kuu ya Uingereza ambao anaichezea klabu ya Everton, Romelu Lukaku amesema anatamani sana kucheza Uefa.

Mchezaji huyo alisema hivyo kupitia mtandao wake wa twitter akitafsiriwa amesema hivyo kwa maana anataka kuhama timu yake ya sasa ya Everton ambayo haitalajiwi kumaliza ndani ya nafasi nne za juu ambapo timu inayomaliza ndani ya nafasi hizo ndiyo inayoshiriki mashindano hayo ya klabu bingwa ya Ulaya.

Mpaka sasa bado kuna fununu kwamba Chelsea inataka kumrudisha tena kikosini baada ya hapo mwanzo kumsajili kutoka Anderlecht kisha tena wakamuuza kwenda Everton ambayo ndiyo anayoichezea kwa sasa ambapo kwa kauli yake hiyo ni kama inaonekana anaweza akarudi tena Stamford Bridge na kuuchukua mshahara wa Abramovich tajiri wa kirusi anayeimiliki timu hiyo matajiri wa London Magharibi.

Lakini pia Juventus na Bayern Munich zinatajwa kuitaka saini ya mchezaji huyo mwenye asili ya kikongo.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.