Friday 10 February 2017

PL: Burnley vs Chelsea

Siku ya jumapili ya tarehe 12-02-2017 kutakuwa na mchezo wa ligi kuu ya Uingereza kati ya Burnley dhidi ya Chelsea ambapo Chelsea watakuwa ugenini kumenyana na timu hiyo inayoshika nafasi ya 12 katika msimamo wa ligi kuu Uingereza.

Na hiki ndo kikosi kinachotazamiwa kucheza.

Raha ya mchezo huu
1. Wanakuta makipa ambao wote wana utamu wao wanalindwa kwa takwimu zao, Tom Heaton ambaye ndie kipa wa Burnley mpaka sasa ndie kipa anaeongoza kwa kuokoa michomo mingi akiwa kaokoa mara 103 wakati Thibaut Courtois kipa wa Chelsea yeye anaongoza kwa kucheza mechi nyingi bila kuruhusu goli. Mechi 13 za ligi kuu.

2. Lakini pia utamu wa mchezo huu, Diego Costa atakutana na timu ya kwanza kuifunga akiwa Uingereza. Ambapo msimu wa 2014-2015 aliifungia Chelsea bao lake la kwanza baada ya kutumia dakika 17.

3. Lakini pia Burnley watataka kuendeleza historia yao nzuri dhidi ya Chelsea ambapo toka wakutane Burnley kashinda michezo 37 na huku Chelsea akishinda 34 na kutoa sare 22.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.