Mchezaji aliyekuwa na msimu mzuri ndani ya Chelsea, Pedro Rodriguez ametoa neno kuhusu ubora wake unaendana vipi na Antonio Conte, kocha mkuu wa timu hiyo.
"mara zote nimekuwa natamani kuonyesha kiwango bora kwa timu yangu, nimekuwa natamani kufunga kila wakati ili kuisaidia timu yangu. Cha muhimu ni kuhakikisha timu inapata mafanikio nami nafurahi kuwa mmoja wa watu muhimu kwa Conte ili kuipatia timu mafanikio" alisema Pedro.
Pedro mpaka sasa kwa msimu huu wa 2016-17 ameichezea Chelsea mechi 24 na kufunga magoli 9 na kutoa pasi za mwisho 7.
No comments:
Post a Comment