Tuesday, 14 February 2017

Mourinho ana wivu

Mchezaji wa zamani wa Manchester united amemtupia kijembe kocha wa Manchester united ambae kabla alikuwa kocha wa Chelsea, Jose Mourinho kwa kusema kocha huyo ana wivu na mafanikio ya Chelsea ambayo kwa sasa ndio inaongoza ligi ikiwa chini ya muitaliano, Antonio Conte.

Jose Mourinho mwishoni mwa wiki iliyopita alikaririwa akisema "itakuwa ngumu kwa timu yoyote kuishinda Chelsea katika mbio zake za kulitwaa taji la ligi kuu, kwa vile Chelsea inacheza soka la kujihami sana"

Ambapo kauli hiyo mchana wa leo imepingwa vikali na mchezaji wa zamani wa Manchester united lakini pia aliyewai kuwa kocha wa Valencia, Gary Neville pale aliposema "ni wivu tu iliyo ndani yake, kiupande wangu naona Chelsea inacheza soka bora na lililobalance katika kushambulia na kukaba pia"

Jose Mourinho ndie kocha aliyeipatia mafanikio makubwa klabu ya Chelsea kuliko kocha yeyote kuwai kutokea.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.