Jina kamili; Diego da Silva Costa
Siku ya kuzaliwa; 7-October-1988
Miaka kwa sasa; 28
Mahali alipozaliwa; Lagardo, Brazil
Urefu; mita 1.88 (futi 6 na inchi 2)
Nafasi anayocheza; Mshambuliaji
Klabu anayoichezea; Chelsea
Namba ya mgongoni; 19
Baba yake anaitwa Jose de Jesus na mama yake Josileide. Baba yake alimuita Diego kwa kutokana na mapenzi yake kwa mchezaji zamani wa Argentina, Diego Maradona na pia Diego Costa ana kaka yake anayeitwa Jair ambapo pia baba yake alimuita ivo kutokana na mahaba yake kwa mchezaji wa kibrazil, Jairzinho.
Wakati akiwa na miaka 15 alihama kutoka mahali alipokuwa anaishi katika kitongoji cha Sergipe na kwenda Sao Paulo kwa mjomba wake aliyeitwa Jarminho. Ambaye alikuwa na kama store ambapo pia Costa alikuwa akimsaidia kufanya kazi za pale.
Wakati akiwa kwa mjomba wake huyo ambaye alikuwa ana watu anafahamiana nao kwenye soka ndipo mjomba wake akamsaidia kuungana na timu ya Barcelona EC ambayo ndio ilikuwa timu yake ya kwanza kuichezea kabla ya kuungana na Braga ya Ureno mwaka 2006.
Baada ya kuichezea Braga usajili uliosaidiwa kwa asilimia kubwa na Jorge Mendes wakala ambaye anawasimamia wachezaji wakubwa akiwemo Cristiano Ronaldo na hata Jose Mourinho hakukaa sana hapo Braga na ndipo akasajiliwa na Atletico Madrid mwaka 2007 lakini hakuichezea mechi hata moja na akatolewa kwa mikopo na kuzichezea timu nne tofauti akiwa kwa mkopo kabla ya mwaka 2009 kusajiliwa na Valladolid.
Lakini pia alikaa Valladolid sio muda mrefu kisha mwaka 2010 akasajiliwa tena na Atletico Madrid ambayo aliichezea kabla ya mwaka 2014 alipoenda tena Rayo Vallecano kwa mkopo na kuichezea michezo 16 na kufunga mabao 10 kabla ya kurudishwa tena Atletico Madrid na mpaka anaondoka klabuni hapo aliichezea michezo 94 na kufunga magoli 47.
Maisha yake ndani ya Chelsea yalianza mwaka 2014 ambapo alisajiliwa na Mourinho ambapo katika msimu wake wa kwanza alifanikiwa kuifungia Chelsea mabao 21 na kufanikiwa kutwaa makombe mawili ndani ya msimu huo huo wa 2014-2015. Alitwaa taji la ligi kuu Uingereza na kombe moja la kombe la ligi (Capital cup ambalo kwa sasa linaitwa EFL)
Mpaka sasa akiwa na uzi wa Chelsea amefanikiwa kuichezea michezo 78 na kufunga mabao 48 akiwa na uwiano wa kufunga 0.615 kwa kila mechi.
Aliichezea Brazil timu yake ya taifa ambalo alizaliwa michezo miwili na hakufanikiwa kuifungia bao lolote kabla ya kuamua kuachana na timu hiyo na kujiunga na Hispania ambayo mpaka sasa ameichezea michezo 14 na kuifungia magoli 4.
Mpaka sasa amecheza michezo 381 na kufunga magoli 160.
No comments:
Post a Comment