Mpaka sasa hakuna taarifa za uhakika kwamba David Luiz atarudi mchezoni katika mechi ya Jumamosi dhidi ya Swansea baada ya daktari ambaye ndiye anayemhudumia kutotoa neno la mwisho juu ya kama Luiz atakuwepo au hatokuwepo.
Luiz ambaye alipata majeraha ya goti la mguu wa kulia miezi mitatu nyuma baada ya kuchezewa rafu mbaya na Kun Aguero katika mchezo dhidi ya Man city lakini alikuwa akiendelea kucheza japo alikuwa majeruhi.
Mchezo uliopita hakusafiri na timu kabisa ambapo Chelsea ilicheza mchezo wa raundi ya tano dhidi ya Wolves mchezo ulioisha kwa Chelsea kushinda 2-0 na kufanikiwa kufuzu kuelekea robo fainali itakapocheza dhidi ya Manchester united mwezi March tarehe 13 ambapo Luiz aliachwa ili kupatiwa matibabu zaidi.
Lakini haijathibitishwa kama atakuwa amepona zaidi kuweza kurudi tena mchezoni.
Kwa iyo mpaka sasa kinachosubiriwa ni mkutano wa Conte siku ya ijumaa ili kutoa neno la mwisho kutoka kwa daktari kama Luiz atacheza au laah.
No comments:
Post a Comment