Friday, 24 February 2017

Antonio Conte kwenye mkutano tarehe 24-February-2017

Leo kama kawaida yake mchana wa leo Antonio Conte amekutana na waandishi wa habari katika mkutano. Na haya ndiyo aliyoyasema;

Kuhusu Ranieri
Conte; Nina huzuni sana kwa yaliyotokea. Namuelewa Ranieri na kwangu ni kama rafiki.

Kuhusu kutimuliwa kwa Ranieri
Conte; Nadhani Leicester hawajafanya jambo la kiungwana namuheshimu Ranieri na naona hawajamtendea haki.

Kuhusu Mancini kuichukua Leicester
Conte; Namheshimu Roberto Mancini na sizani kama itakuwa sahihi kuliongelea hili wakati rafiki yangu (Ranieri) ametoka kufukuzwa muda mfupi uliopita

Kuhusu kukutana na Swansea na (Paul) Clement
Conte; Naamini utakuwa mchezo mgumu kwetu lakini kikubwa nina imani na wachezaji wangu. Clement (kocha wa Swansea) amekuwa na mafanikio katika michezo iliyopita na nina imani ataisukuma timu yake ipambane zaidi

Kuhusu Llorente
Conte; Namjua Llorente, nimekuwa naye Juventus. Ni mchezaji bora na namhusudu sana. Nadhani tutacheza kuyazuia mashambulizi yake na timu kwa ujumla. Kikubwa tunawajua Sigurdsson, Fer na Llorente pia.

Kuhusu kujaribu kumsajili Llorente
Conte; Navutiwa naye na nilijaribu kumsajili nadhani hiyo ishapita na haina haja ya kuizungumzia sana.

Kuhusu kutokuwepo Uefa na Ueropa
Conte; sio jambo zuri, wachezaji wanataka kucheza kati ya wiki na hata benchi la ufundi pia linatamani hilo lakini nadhani ni jambo zuri kwa kocha mgeni kuwa na timu kwa wiki nzima

Kuhusu kupangwa na Man utd katika FA Cup
Conte; sidhani kama ni sahihi kulizungumzia hilo wakati kuna siku 18 mpaka kuufikia mchezo huo.

Kuhusu Leicester
Conte; Jambo pekee naloliona ni kwamba Leicester hawajamtendea haki (Ranieri). Alikuwa nao akawapa taji lakini leo wanamdhalilisha kwa waliomfanyia. Nitaongea nae, nadhani sio muda nitampigia kuongea nae.

Kuhusu mchezo wa 1000 kwa Ancelloti
Conte; Ni jambo jema kwake na nampongeza kwa hilo ni heshima kwake kwa kufikia mafanikio hayo.

Kuhusu majeruhi ndani ya Chelsea
Conte; Hakuna majeruhi yoyote

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.