Mpaka sasa hivi inaaminika kiungo wa Barcelona ya nchini Hispania ni kama anatarajia kutua Chelsea mwishoni mwa msimu huu.
Kiungo huyo ambaye amekuwa hafurahishwi na maisha ya Barcelona katika kitongoji cha Cataluna alikuwa akihusishwa na kutua Chelsea lakini fununu hizo zimeonogezwa baada ya kudaiwa kununua nyumba katika jiji la London ambao ndio jiji makazi ya klabu ya Chelsea.
Bado haijadhihirika kwa asilimia zote kwamba msimu ujao atatua Chelsea lakini kutokana na picha zake ambazo amekuwa akipiga akionekana kuwa na Diego Costa ambaye alicheza nae timu moja ya Atletico Madrid kabla ya Costa kuja Chelsea na yeye kutimkia zake Barcelona.
Na kwa kununua kwake nyumba katika jiji la London ni kama kumezidi kuchochea.
No comments:
Post a Comment