Kiungo wa Barcelona, Arda Turan ametajwa kuhusika na tetesi za kutua Stamford Bridge katika dirisha kubwa la usajili mwishoni mwa msimu.
Kiungo huyo ambaye alisajiliwa akitokea Atletico Madrid kwa dau la paundi milioni 24 ametajwa kutokua na furaha katika timu hiyo wababe wa Hispania akiwa amecheza michezo 34 tu katika timu hiyo na kwa maana hiyo ametajwa kuhusika na kutua Chelsea.
No comments:
Post a Comment