Friday 10 February 2017

Antonio Conte kwenye mkutano

Antonio Conte kocha mkuu wa Chelsea amefanya mkutano na waandishi habari mchana wa leo kuelekea weekend ya muendelezo wa ligi kuu.

Kuhusu Eden Hazard kutakiwa
Conte; nadhani ni mchezaji mzuri na anaonekana anacheza vizuri muda wote hilo halina ubishi lakini sizani kama anauzwa.
*Akimaanisha Hazard hauzwi hii ni taarifa kwa Real Madrid na timu zinazomfukuzia.

Kuhusu mchezo dhidi ya Burnley
Conte: ni mchezo mzuri na Burnley wamekuwa na matokeo mazuri haswa wakiwa nyumbani, naamini wachezaji wangu watafanya kile kinachowapasa. Cha muhimu kuondoka na ushindi
*Nawaambia tu yule Tom Heaton pale golini ajiandae tu maana huu moto wa Chelsea sio wa mchezo

Kuhusu kuukaribia ubingwa
Conte: ni kweli tupo vizuri lakini hii isiwafanye wachezaji wangu wajisahau hapana bado tuna safari ndefu mbele yetu
*haters msituchukie yani hapa ni mwendo wa vipigo tu

Kuhusu Fabregas na Willian
Conte: ni wachezaji bora lakini sioni tatizo kwa wao kukaa benchi nadhani Pedro amekuwa bora sana
*yani hii Chelsea anatoka changarawe anaingia kokoto

Kuhusu safari yake alipoenda Juventus
Conte: ile haikuwa na maana yoyote zaidi ya kwenda kusafisha akili (relax) na kutoa uchovu. Nilienda kama matembezini tu
*ndo raha ya ushindi na kuwa bora unadhani leo eti Wenger asafiri bila mpango ataeleweka?

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.