Friday, 17 February 2017

Antonio Conte akiwa kwenye mkutano 17-February

Mchana wa leo kama ilivyo kawaida ya Antonio Conte kukutana na jopo la waandishi wa habari kuzungumzia kuhusu timu na yale yote yanayoihusu.

Kuhusu John Terry
Conte; John Terry yupo sawa yeye na wachezaji wote lakini nadhani ingekuwa sahihi Marcos Alonso na David Luiz wangepata muda zaidi wa kupumzika.
*hii ni kama inamaanisha Luiz na Alonso hawatosafiri pamoja na timu.

Kuhusu David Luiz
Conte; Nadhani anaendelea vizu GGiri. Nami naliona hilo. Na ukimwangalia goti lake kwa sasa na baada ya mchezo wa Man city ni tofauti. Inamaanisha anaendelea kuimarika na kuwa sawa zaidi.
*hii inamaanisha kwenye mchezo wa ligi kuu unaokuja dhidi ya Swansea basi Luiz atakuwa sawa huenda kwa 100%

Kuhusu FA Cup
Conte; Ukiwa kama kocha au mchezaji wa Chelsea basi ni lazima uwe unatamani kushinda kwa kila taji.
*jamaa hadharau kombe lolote anachezesha kama kawaida.

Kuhusu Diego Costa
Conte; sizani kama itakuwa sahihi kuongelea kama ataweza kubaki au kuondoka kwa sasa. Hiki sio kipindi cha usajili cha muhimu ni kuongelea na kushughulika na mechi inayofata (vs Wolves) ya kesho.
*kila jambo na wakati wake kwa sasa tunaangalia mechi itakuwaje na sio kuangalia nani ataondokaje! yah nimemwelewa Conte hataki masikhara na kombe lolote.

Kuhusu Arsene Wenger
Conte; nadhani yeye ni mmoja kati ya makocha bora duniani.
*hahaaaa! Arsenal jamani mpendeni kibabu chenu.

Kuhusu Dominic Solanke

Conte; Nadhani ana kipaji lakini pia ana maamuzi yake ambaye hakuna mtu wa kumuingilia. Kiusahihi mkataba wake unaisha mwezi wa sita mwaka huu namimi nitajaribu kukaa nae chini kama kocha na kuongea nae.

*Solanke anatajwa kujihusisha na usajili wa kwenda Liverpool ambapo anaamini atapata nafasi zaidi ya kucheza kikosi cha kwanza.


Kuhusu Clattenburg

Conte; ni habari mbaya. Ye ni refa bora na anahitajika sana kwenye ligi na naamini ingekuwa sahihi kama nchi ingeendelea kubaki na kitu bora.

*Clattenburg inasemekana ataachana na soka la Uingereza kabla ya raundi inayofata ya ligi kuu.


Kuhusu Shule ya soka ya Chelsea

Conte; ni jambo zuri tena sana kuwa na hii shule maana inatoa wachezaji waliobora. Nina Chalobah, Ake, Ruben na Aina katika timu ya wakubwa ambao wote hao wametoa katika shule hiyo.

*ikumbukwe tena kuwa na shule kama hiyo itasaidia kupunguza gharama za timu kusajili wachezaji kwa bei kubwa.


Kuhusu Charly Musonda

Conte; hatocheza mechi ya kesho. Bado sijaona kama yupo tayari kucheza katika timu ya wakubwa. Bado ana kazi ya kufanya. Na kesho atakuwepo kwenye mchezo wa Chelsea U23 ambao watacheza dhidi ya Man city U23

*mmmhh! Musonda anatajwa kuwa moja kati ya kizazi cha dhahabu akiwa na kipaji kikubwa.


Kuhusu hali ya ushindi

Conte; kila kocha anatamani kuona timu yake ikiwa kwenye hali hiyo ya kushinda kila mchezo na naamini timu yangu wapo kwenye hali hiyo.

*mechi ya kesho dhidi ya Wolves, sisi kama mashabiki wa Chelsea tunategemea kuona magoli mengi tukifunga na kucheza soka la hali ya juu.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.