Toka atoke kwa mkopo alipokuwa AFC Bournemouth, Nathan Ake hajawai kuanza mechi yeyote zaidi ya mchezo wa jumamosi kati ya Chelsea na Wolves na alicheza vizuri mpaka BBC Sport wakampa uwiano wa 3.5 katika mchezo huo.
Baadhi ya mashabiki wa Chelsea wamekuwa wakiamini Ake ana kiwango bora zaidi ya Marcos Alonso ambaye naye amesajiliwa akitokea Fiorentina ambapo kwa sasa amekuwa kwenye kikosi cha kwanza cha Conte. Lakini mashabiki wanaamini inapaswa Conte amwamini Ake maana ana kiwango kizuri zaidi ya Alonso.
Ake amekuwa akipata wakati mgumu toka aliporudi Chelsea akitokea kwa mkopo Bournemouth ambapo huko alikuwa akicheza haswa kama mlinzi wa kati nafasi ambaye kwa Chelsea inaonekana haina pengo maana kuna Luiz, Azpilicueta na Cahill wanaoonekana kuelewana zaidi na mpaka sasa wakiwa wameruhusu magoli 18 tu katika mashindano yote.
Je unadhani ni sahihi kwa Ake kuchukua nafasi ya Alonso?
No comments:
Post a Comment