Monday, 13 March 2017

FA Cup; Chelsea vs Man utd 13-March-2017

Historia
Chelsea na Man utd wamekutana mara 175 na Chelsea imefanikiwa kushinda mara 51 na kupoteza mara 75 na kutoka suluhu mara 49.
Mchezo wa kwanza baina ya Chelsea dhidi ya Man utd ulichezwa tarehe 25-December-1905 ambayo ilikuwa siku ya Christmas na kuisha kwa suluhu ya bila kufungana ambapo mchezo huo ulichezwa katika uwanja wa Bank Street uliokuwa Clayton na mashabiki 35,000 kufanikiwa kuishuhudia mechi hiyo wakiwa uwanjani.
Mchezo wa mwisho kwa timu hizo kukutana ilikuwa 23-October-2016 na Chelsea kufanikiwa kuibamiza Man utd jumla ya magoli 4-0 katika mchezo wa ligi kuu na kuruhusu jumla ya mashabiki 41,424 kuingia katika uwanja wa Stamford Bridge kuutazama mchezo huo.

Habari za timu
Chelsea; Kwa upande wa Chelsea hakuna jambo jipya na wachezaji wote hakuna aliyeripotiwa kuwa ni majeruhi

Man utd; Kwa upande wa mashetani wekundu watawakosa Rooney ambaye alipata ajali mazoezini baada ya kuchezewa vibaya na Phil Jones, Anthony Martial ambaye naye ameripotiwa kuwa ni majeruhi, Rashford ameripotiwa kwamba naye ni mgonjwa na wakati Ibrahimovic ataanza adhabu yake ya kufungiwa michezo mitatu baada ya kumpiga kiwiko mchezaji wa Bournemouth.

Makocha wanasemaje
Conte; Kabla ya mchezo wa October (mchezo wa mwisho kwa timu hizo kukutana) nilikuwa naiona Man utd ni timu kubwa. Hata sasa bado naiona timu kubwa, ni kama Man city tu zote zina vikosi bora. Tunacheza soka safi na zuri pia nadhani utakuwa mchezo mgumu haswa tunapokutana na timu bora. Napenda kufanya kwa vitendo zaidi kuliko maneno na hicho ndicho kinachotakiwa. Kwa maana hiyo sitoongea sana sasa nataka tuongee baada ya mchezo.

Mourinho; Hatuwezi kwenda na kikosi cha vijana wa miaka chini ya 23. Man utd ina kikosi kikubwa sana. Lakini pia ndie bingwa wa kombe hili. Sio kosa la Chelsea kwa mchezo wa leo jumatatu lakini inatakiwa tufanye mabadiliko ya uhakika zaidi

5 vs 5
Chelsea
-Chelsea wameshinda michezo 15 kati ya 16 waliocheza uwanja wao wa nyumbani chini ya Conte katika mashindano yote
-Chelsea wameshinda michezo 9 kati ya 10 ya kombe la FA wakiwa uwanja wao wa nyumbani
-Chelsea imefika robo fainali ya kombe la FA mara nyingi zaidi katika karne ya 21. Wamefika mara 12.
-Pedro amefunga katika kila hatua ya kombe hilo ambapo mpaka sasa ana magoli 4 na pasi za mwisho 2
-Mara ya mwisho Chelsea kumfunga bingwa mtetezi wa kombe hilo ilikuwa mwaka 1966 dhidi ya Liverpool kwa bao 1-0.

Man utd
-Mara ya mwisho Man utd kupoteza nje ya uwanja wake wa Old Trafford alifungwa 1-0 dhidi ya Chelsea mwaka 2013
-Jose Mourinho ambaye ndie kocha wa Man utd hajawai kutolewa katika hatua ya robo fainali ya FA.
-Kipigo cha 4-0 ndicho kipigo alichokipata Mourinho kikubwa toka afike kwenye ligi ya Uingereza.
-Rashford ambaye leo hatocheza ameifungia timu yake magoli 6 katika kombe hilo la FA.
-Huu ni mchezo wa 46 kwa Man utd katika mechi za kimashindano wakati kwa Chelsea huu ni mchezo wake wa 34 kwa msimu huu.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.