Monday 13 February 2017

Yaliyotokea Burnley vs Chelsea

Haya ndio mambo au record zilizowekwa ama kuvunjwa katika mchezo kati ya Burnley vs Chelsea tarehe 12-February-2017 ulioisha kwa suluhu ya 1-1

>Burnley wamefanikiwa kucheza michezo sita bila kufungwa wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani ambapo mara ya mwisho kufanya hivo ilikuwa Septemba 1975, kwa maana hiyo imepita miaka 41 na miezi 5.

>Chelsea ndio timu pekee iliyoshinda magoli mengi ya kuongoza, magoli 19 na katika kutangulia uko kwa magoli hawajapoteza mchezo hata mmoja. Wameshinda 16 na kusuluhu 3.

>Pedro katika msimu huu wa 2016-17 ameifungia Chelsea magoli 9 katika michuano yote ambayo ni magoli mengi kuliko yale aliyoifungia timu hiyo msimu wa 2015-16 ambapo aliifungia magoli 8.

>Robbie Brady ni mchezaji wa kwanza kufunga mpira wa adhabu wa moja kwa moja dhidi ya Chelsea katika ligi kuu ya Uingereza toka alipofanya hivyo Rickie Lambert katika mwezi March 2013.


>Brady ni mchezaji wa tatu wa Burnley kufunga goli katika mechi yake ya kwanza akiungana na Scott Arfield mwaka 2014 na Daniel Fox mwaka 2010.


>Diego Costa ameshindwa kufunga goli lolote katika mechi 3 mfululizo ambapo mara ya mwisho kufanya hivyo ilikuwa April-May 2016.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.