Jumamosi hii pale darajani itakuwa ya kuvutia sana.
Ukiachana na mchezo wa ligi kuu ambao ndio utakuwa moja ya chanzo cha upekee na utamu wa mechi hiyo kuzidi lakini kuna mengi yataenda kutokea.
Makelele kutua Stamford Bridge kwa mara ya kwanza kama kocha. Claude Makelele ambaye ndie kocha msaidizi wa Swansea atatua Chelsea kwa mara ya kwanza toka alivyoondoka akiwa kama mchezaji wa Chelsea na mara hii anarudi akiwa kama kocha.
Frank Lampard kuingia uwanjani. Moja kati ya jambo linalosubiriwa kwa hamu ni pale Frank Lampard akirudi tena darajani na kukwaa jukwaa kuu kama mmoja ya wageni muhimu lakini kubwa zaidi ni pale atakaposhuka kutoka jukwaani na kuingia uwanjani na kuwasalimia mashabiki wakati wa mapumziko.
Malegend kukutana. Mchezo huu utakuwa ayo yakitokea lakini kile kiungo bora kuwai kutokea Uingereza kwa kuwasaidia mabeki lakini kuzidisha mashambulizi kilichowajumuisha Makelele na Lampard kitaenda kuwakutanisha tena baada ya muda mrefu kupita ambapo mara ya mwisho wote walikuwa wachezaji.
Chelsea kutaka kutengeneza tofauti kubwa. Kwa sasa Chelsea inapigana ili kujihakikishia kupata taji mapema, kwa iyo katika mchezo huu Chelsea watataka kupata goli mapema lakini pia na Swansea hawapo pazuri kwenye msimamo wa ligi kuu. Atataka ashinde ili atoke kwenye eneo jekundu la hatari.
No comments:
Post a Comment